📘 Logistics Tips
01 Apr 2026 · Doctor Cargo Team
Kwa nini mizigo ya vilipukizi / sensitiv inaweza kuchukua muda mrefu kufika Tanzania?
Aerosol, spray, na bidhaa zenye shinikizo huenda zikahitaji njia maalum (DG) badala ya ndege ya moja kwa moja.
Bidhaa nyingi za kila siku — deodorant, spray ya nywele, baadhi ya vilegera — zinaainishwa kama mizigo hatari au restricted kwenye ndege nyingi za moja kwa moja.
Inamaanisha nini?
Badala ya mstari mfupi wa moja kwa moja, mzigo unaweza kupitia hub maalum, ukaguzi wa ziada, na nafasi ndogo ya cargo — hivyo muda wa juu wa siku 7–10 ni wa kawaida kwa kategoria hizi.
Unachoweza kufanya
- Eleza mapema ni bidhaa gani unazoagiza
- Usifiche ingredients za shinikizo au moto
- Uliza quotation ya njia ya DG kabla ya kununua kwa wingi
Tuna huduma maalum kwa mizigo hii kupitia Dangerous goods route — angalia maelezo ya njia na muda.